Alhamisi, Mei 18, 2017

MVUA YAFANYA UHARIBIFU RUVU, SAFARI ZA TRENI ZASIMAMISHWA

Uongozi Kampuni ya Reli Tanzania (TRL) umetangaza kusimamishwa huduma ya treni za abiria kutoka Dar es Salaam kwenda bara kuanzia leo Mei 18, 2017 hadi itakapotangazwa tena.
Uamuzi huo umechukuliwa baada ya kutokea uharibifu wa miundombinu ya reli leo asubuhi kati ya stesheni za Ruvu na Ruvu junction uliosababishwa na mvua kubwa zinazonyeshwa maeneo hayo ya mkoa wa Pwani.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo ya kusitisha huduma kwa muda treni ya abiria ya deluxe iliokuwa iondoke Dar es Salaam leo saa 2 asubuhi imefutwa na abiria wametakliwa wafike stesheni ili warejeshewe fedha zao za nauli.
Wakati huo huo Uongozi wa TRL tayari umeelekea eneo la tukio ili kufanya tathmini na kupanga mikakati ya haraka kukarabati miundo mbinu husika likiwemo daraja la Ruvu.
Aidha Uongozi umefafanua katika taarifa yake kuwa katika kipindi cha mpito, treni ya abiria kutoka Kigoma na Mwanza kuja Dar es Salaam itaishia Morogoro hadi njia ya reli kati ya Dar es Salaam na Morogoro itakapofunguliwa tena.

0 comments:

Chapisha Maoni