Alhamisi, Mei 18, 2017

AKAMATWA NA POLISI KWA KUAONESHA WATOTO WADOGO VIDEO ZA NGONO

Polisi wa mjini Nakuru ndani ya Kenya wamemtia mbaroni bwana wa miaka 45 ambaye amekutwa na tuhuma za kuwaonesha watoto wadogo wa shule  wa miaka 9-10 video za ngono.
Thomas Musabili ndiye mtuhumiwa aliyekubwa na kasheshe hilo wakati akifahami ni kinyume na sheria za nchi ya kenya vido za aina hiyo kwa watoto wadogo.
Afisa mkuu wa polisi kutokaNakuru, Joshua Omukata amesema askari wake walifanya operesheni ya kumkamata bwana huyo baada ya kupata taarifa za bwana huyo kutoka kwa wasamaria wema kwamba watoto wadogo wamekuwa na mazoea ya kwenda katika nyumba ya mtuhumiwa majira ya saa 9.00 alasiri kila siku kwaajili ya kuangalia video hizo.

0 comments:

Chapisha Maoni