Jaji mmoja wa Mahakama ya Shirikisho ya jimbo la
Kentucky la nchini Marekani amemtuhumu Rais Donald Trump wa nchi hiyo
kuwa alichochea machafuko wakati wa kampeni za uchaguzi.
Hata hivyo kwa mujibu wa Press
TV, David G. Hill, jaji wa mahakama moja ya shirikisho la Marekani huko
Kentucky amesema kuwa, Donald Trump amekanusha madai yaliyotolewa dhidi
yake ya kwamba alichochea machafuko wakati wa kampeni za uchaguzi mwaka
2016.
Pamoja na hayo, jaji huyo ametoa hukumu
inayoruhusu kufuatiliwa mashtaka yaliyofunguliwa dhidi ya Trump na timu
yake ya kampeni.
Jaji huyo wa Mahakama ya Shirikisho ya
Marekani aidha amesema, kuna ushahidi wa kutosha wa kuthibitisha kwamba
kulitokea machafuko wakati wa kampeni za uchaguzi za Donald Trump, na
kusema kwamba rais huyo wa Marekani alisababisha machafuko hayo.
Mawakili wa Donald Trump wamefanya
juhudi za kuzuia kesi za walalamikaji watatu ambao wanasema kuwa, mwezi
Machi 2016 walishambuliwa kwa kupigwa na kutukanwa na wafuasi wa Trump
wakati rais huyo wa Marekani alipokuwa anahutubia wafuasi wake katika
jimbo la Kentucky.
Wanawake wawili na mwanamme mmoja
wamefungua kesi mahakamani dhidi ya Donald Trump wakilalamika kuwa,
walishambuliwa na kutukanwa na wafuasi wa Trump kwa amri ya rais huyo wa
Marekani.
Matamshi ya jaji huyo wa Mahakama ya
Shirikisho ya Marekani ya kwamba Trump alichochea machafuko na kupigwa
walalamikaji hao, linahesabiwa kuwa ni pigo jingine la kisheria kwa rais
huyo mwenye chuki dhidi ya wageni, watu wasio Wazungu na pia dhidi ya
Waislamu.
0 comments:
Chapisha Maoni