Alhamisi, Machi 23, 2017

ZAMBIA YAKABILIANA NA MAKANISA YA WAPIGA DILI

Serikali ya Zambia imetangaza hatua madhubuti ya kukabiliana na ongezeko la makanisa ya wapiga dili nchini humo yakiongozwa na makasisi tapeli wanaohadaa waumini.
Godfridah Sumaili, waziri anayesimamia masuwala ya dini nchini Zambia ameonya kuwa hakuna kanisa litakalosajiliwa bila idhini kutoka kwa wizara yake. Waziri huyo ameongeza kuwa makanisa yote yatalazimika kujiandikisha na msajili wa vyama nchini humo kabla ya kuruhusiwa kuhudumu.
Baadhi ya makanisa na viongozi wao yameripotiwa kuhadaa waumini kuwalipa pesa kwa kisingizio kuwa wana uwezo wa kumaliza matatizo yao. Kumekuwa pia na ripoti za makasisi kutaka kushiriki ngono na waumini na kuahidi kuwafanyia miujiza ya kubadilisha maisha yao.

0 comments:

Chapisha Maoni