Alhamisi, Machi 23, 2017

WANANCHI WA ZAMBIA KUPIGA KURA AMA KUSALIA AU KUJIONDOA ICC

Zambia itakusanya maoni ya umma kuhusu uanachama wa nchi hiyo kwenye mahakama ya kimataifa ya makosa ya jinai ICC. Rais Edgar Lungu wa Zambia amesema serikali itakusanya maoni ya umma kabla ya kufanya uamuzi wowote kuhusu uanachama wa Zambia kwenye mahakama hiyo.
Hatua hiyo ya Zambia inakuja kufuatia azimio lililopitishwa na Umoja wa Afrika kuhusu kujitoa kwa pamoja kutoka mahakama hiyo, licha ya kuwa azimio hilo halibani kisheria.
Waziri wa sheria wa Zambia Bw Given Lubinda amesema maoni yatakusanywa kati ya Machi 27 na Machi 31 kwenye wilaya 30 kati ya 103 za Zambia. Wananchi wataruhusiwa kutoa maoni yao kwa njia ya maandishi.

0 comments:

Chapisha Maoni