Jumamosi, Machi 25, 2017

TAIFA STARS YATOKA KIFUA MBELE DHIDI YA BOTSWANA DA ES SALAAM

Timu ya taifa ya soka ya Tanzania 'Taifa Stars' imefanikiwa kuutumia uwanja wake wa nyumbani vema kwa kutoka kifua mbele dhidi ya timu ya taifa ya soka kutoka nchini Botswana kwa mabao 2-0 jijini Dar es Salaam.
Taifa Stars imeibuka na ushindi huo ikimkosa mchezaji Thomas Ulimwengu anayetajwa kwenda sawa kimchezo na Mbwana Samatta aliyefunga magoli yote mawili katika kipindi cha kwanza na cha pili katika mchezo huo wa kirafiki wa kimataifa.
Jumanne ya wiki ijayo, machi 28, 2017 Taifa Stars itakuwa tena uwanjani, Uwanja wa Taifa kupambana katika mechi nyingine ya kimataifa ya kirafiki na timu ya taifa ya Burundi.
Timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars inahitaji ushindi katima mechi hiyo pia ili kutafuta nafasi ya kupanda katika iwango vya shirikisho la soka ulimwenguni, FIFA ambako Tanzania imekuwa ikiporomoka bila mpangilio.

0 comments:

Chapisha Maoni