Ijumaa, Machi 31, 2017

NIYONZIMA ANASEMAJE KUHUSU MECHI YA YANGA DHIDI YA AZAM KESHO?

Kuelekea kwenye mtanange wa Ligi Kuu Vodacom kati ya Yanga na Azam, Nahodha msaidizi wa timu ya Yanga kiungo mchezeshaji Haruna Niyonzima ameongelea mchezo huo unaotarajiwa kuchezwa kesho katika dimba la Uwanja wa Taifa. 
Niyonzima amesema kuwa wao kama wachezaji wamejiandaa vyema kisaikolojia kushinda mchezo wa kesho dhidi ya Azam ili kuzipata alama tatu muhimu katika harakati za kulitetea kombe lao wanalolishikilia . " namshukuru mungu binafsi nipo vyema kwa ajili ya mchezo wa kesho, mwalimu akinipa nafasi hakika nitatimiza majukumu yangu vyema pamoja na wenzangu ili kuhakikisha timu yetu inashinda ,"amesema Niyonzima Amesema kuwa waalimu wanawaandaa vyema kushinda mchezo huo na mingine iliyobaki ili kuhakikisha tunatetea ubingwa wetu . 
Niyonzima alienda mbali zaidi kwa kuwataka mashabiki wa timu hiyo kujitokeza kwa wingi kuwapa sapoti ili kuwatia nguvu kwa dakika zote 90. " naheshimu sana mchango wa mashabiki wetu katika timu hii na kulitambua hilo nawaomba kesho wajitokeze kwa wingi ili kutupa sapoti , ari na nguvu ya kupambana muda wote wa dakika 90 dhidi ya Azam FC kwani ni timu nzuri na sote tunajuana vyema hivyo umakini unahitajika katika kuwakabili, "amesema Niyonzima. 
Yanga itawakosa mabeki wake wawili Hassan Kessy na Kelvin Yondani kwa kuwa na kadi tatu za njano ila mpaka sasa uhakika wa washambuliaji wake wawili Mzimbabwe Donald Ngoma na Mrundi Amisi Tambwe ambao bado ni majeruhi wa goti. 
Yanga kesho tarehe 1 , April watakuwa uwanja wa taifa kupepetana na Azam FC katika mchezo wa 25 wa ligi kuu Tanzania bara kuelekea ukingoni mwa ligi hiyo.

0 comments:

Chapisha Maoni