Alhamisi, Machi 30, 2017

MADAKTARI WA CHINA WALIVYOUMBA SIKIO KUTOKA KATIKA MKONO WA MWANADAMU

Madaktari wa upasuaji nchini China wamefaulu kuumba sikio jipya kutoka sehemu ya mkono wa mgonjwa aliyepoteza sikio lake kwenye ajali mbaya ya barabara na kisha kupandikiza sikio hilo jipya kwenye kichwa chake.
Upasuaji huo uliofanywa na madaktari wa chuo kikuu cha Xi'an Jiaotong katika mkoa wa Shaanxi, kaskazini magharibi mwa China- uligawanywa mara tatu. Katika hatua ya kwanza, puto iliyojazwa na maji ya chumvi iliingizwa chini ya ngozi kwenye mkono wa mgonjwa ili kuwezesha sehemu hiyo ya ngozi kukua zaidi. 
Katika hatua ya pili, madaktari hao walikata kipande cha ufupa mwororo kutoka ubavuni mwa mgonjwa na kuuchonga kama sikio kabla ya kuuweka chini ya ngozi katika sehemu ilipotolewa puto ili sikio hilo ikue vizuri.
Dkt Guo Shuzhong aliyeongoza upasuaji huo pamoja na wenzake jana (Jumatano) walipandikiza sikio hilo jipya kwenye kichwa cha mgonjwa huyo katika operesheni iliyochukua muda wa masaa saba. Dkt Guo alisema kuwa upasuaji huo ulikuwa mgumu zaidi kwa kuwa iliwabidi kutafuta mishipia ya damu katika sehemu ambapo sikio la kwanza lilitoka na kisha kuiunganisha mishipa hiyo na sikio jipya.

0 comments:

Chapisha Maoni