Jumatatu, Machi 13, 2017

KUMBE MAKONDA YUKO NCHINI??!! AMEIZINDUA BARABARA HII LEO

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, amezindua barabara ya Barabara ya Bandari via Kidongo Chekundu, iliyopo Kurasini ndio kiungo kikubwa kwa upande wa bandari yetu hapa nchini.
Ombi la ujenzi wa miundo mbinu ya barabara hiyo lilitolewa na Mkuu huyo wa Mkoa miezi miwili iliyopita kwa kampuni ya ujenzi ya kizalendo ya Grant Tech Company ya hapa jijini.

Barabara hiyo aliyoizindua leo Makonda ina urefu wa kilomita moja na imejengwa kwa kiwango cha zege na imegharimu takribani kiasi cha Tsh. milioni 750.
Makonda amemshukuru mkandarasi huyo kwa uzalendo wake na kujitoa kwake kuijenga Dar es salaam kwani kwa kufanya hivyo ndoto ya Mh  Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dr John Pombe Magufuli ya kukuza uchumi na kufikia Tanzania ya viwanda  inaendelea kutimia.
Pia Makonda ametoa onyo kali kwa kampuni za ukandarasi zinazofanya shughuli zao hapa jijini chini ya viwango ya kuwa  kuanzia sasa kampuni hizo pale zitakapotambuliwa zitatakiwa kurudia miradi hiyo kwa gharama zao binafsi na kupewa adhabu ya kufungiwa kandarasi yoyote hapa jijini  kwa miaka mitatu.
“Wananchi wamechoka kutengeneza magari kila mara kutokana na ubovu wa barabara, wakina mama wamekuwa wakijifungulia barabarani hasa nyakati za mvua kama hizi kutokana na ubovu wa barabara zilizojengwa hata miezi 6 haijapita,” 
alisema Makonda.
Hata hivyo, taarifa zilizosambaa siku za hivi karibuni zilidai kuwa Makonda amekwenda mapumziko nchini Afrka Kusini ambako angekaa kwa miezi miwili.

0 comments:

Chapisha Maoni