1. Jumla ya marejesho ya mkopo kwa mwezi yasizidi asilimia kati ya 20 na 40 ya mapato kwa mwezi, lakini ili kuweza kurejesha mkopo bila shida ni vema kuhakikisha marejesho hayazidi asilimia 20. Kama inabidi kuchukua mkopo mkubwa, kipato ni lazima kiongezeke kwanza.
2. Usiruhusu marejesho ya mkopo yakuzuie kulipia mahitaji ya lazima kama chakula, kodi ya pango, ada ya shule na mahitaji mengine muhimu. Kama utashindwa kulipia mahitaji ya lazima ili kuweza kulipia marejesho, usichukue mkopo.
3. Hakikisha una mpango maalum wa jinsi utakavyolipa marejesho iwapo fedha ya mkopo haitaweza kuzalisha mapato ya kutosha kujilipia marejesho
4. Weka rekodi ya kiasi cha marejesho na tarehe ze marejesho ili usichelewe au kukosa kulipa
5. Usitumie fedha ya mkopo kwa kununua mahitaji binafsi yasiyoongeza kipato, hii itakufanya ushindwa kulipa marejesho na kama uliweka dhamana utapoteza mali hiyo.
MUHIMU: Tafakari kwanza kabla ya kuchukua mkopo...
(a) Kama una njia mbadala za kupata fedha unayohitaji, usichukue mkopo
(b) Kama hutaweza kulipia marejesho, usichukue mkopo
(c) Kama hujui utazitumia hizo fedha kufanyia nini, usichukue mkopo
0 comments:
Chapisha Maoni