Alhamisi, Machi 16, 2017

IWAPO TUNDU LISSU ATAZUILIWA MAHABUSU, UCHAGUZI WA TLS UTAFANYIKA HIVI KISHERIA

Kanuni za Uchaguzi TLS zinaruhusu Mgombea kuchaguliwa/kupigiwa kura hata kama hayupo ukumbini wakati wa Uchaguzi/kupiga kura.
Kuna precedent pia katika chaguzi katika ngazi za chapters mbalimbali hivi karibuni; ambapo wagombea walipigiwa kura licha ya kutokuwepo ukumbini wakati wa uchaguzi/kupiga kura.
Sisi ni Wanasheria na tuna jukumu la kuzitumia sheria na kanuni zetu za Uchaguzi katika namna itakayosaidia kutatua matatizo kama ya kukamatwa kwa Antipas Tundu Lissu Mughwai anayegombea nafasi ya Rais wa TLS.
Kukamatwa kwake Tundu Lissu hakuzuii yeye kupigiwa kura na kuchaguliwa kuwa Rais wa TLS.
Wanasheria mnaopanga kuja Arusha mje kwa wingi wenu kama mlivyopanga, na tushirikiane kuhakikisha Uchaguzi utafanyika kwa amani na utulivu kama ilivyo ada yetu Wanasheria. Case iliyofunguliwa na Bw. Onesmo Mpinzile vs TLS na AG kuhusiana na Uchaguzi huu imetupwa leo na Panel ya 3Judges kama mlivyosikia.

Kuhusu kukamatwa kwa Tundu Lissu;

Baada ya kuachiwa kwa dhamana kufuatia kukamatwa kwake Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu alipofutiwa Mashtaka ya Uchochezi, alitakiwa ku-report Police DZPZ J3 13th March 2017. Siku hiyo Lissu alikuwa Dodoma katika case aliyofungua Bw. Godfrey Wasonga vs TLS na A.G.

Mdhamini wa Lissu, Wakili Nashon Nkhungu, alifika Central Police Station 13th March akiwa nami na Wakili Omary Msemo na kutoa taarifa kwa Uongozi wa DSPZ kwamba Lissu ana udhuru wa kiMahakama huko Dodoma. Ikaamriwa a-report leo Alhamisi 16th March.
Leo Alhamisi 16th March mdhamini wa Lissu, Wakili Nashon Nkhungu, alifika tena Central Police Station na kutoa taarifa kwa Uongozi wa DSPZ kwamba Lissu yuko Dodoma ambapo anaendelea na case iliyofunguliwa na Bw. Wasonga ambayo inaendelea leo 16th March saa 4 asubuhi, na kisha saa 9 alaasiri. Madai ya kuruka dhamana Lissu hayawezi kuwa na msingi katika premises hizo.
Tunaamini busara itatumika na Tundu Lissu ataachiwa na kuamriwa afike Polisi baada ya case ya Mahakama Kuu Dodoma, na kisha Uchaguzi wa TLS ili kukidhi matakwa yoyote yale ya kichunguzi/arraignment in court kama ambavyo amekuwa akifanya kila mara huko nyuma.
Lakini kama Polisi wakiona ni busara zaidi kumshikilia Lissu; tutafanya kila tuwezalo kisheria ndani ya kanuni za Uchaguzi TLS ili kumpigia kura in absentia kwa mujibu wa kanuni kama ilivyosemwa hapo juu.

Imeandikwa na Peter Kibatala

0 comments:

Chapisha Maoni