Alhamisi, Machi 16, 2017

TUNDU LISSU AKAMATWA NA POLISI DODOMA LEO, ASAFIRISHWA KWENDA DAR ES SALAAM

Kuna taarifa za Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu kukamatwa na jeshi la polisi asubuhi ya leo mkoani Dodoma, hii ni kwa mujibu wa kile alichokiandika katika mitandao ya kijamii mapema leo, nanukuu maneno yake;
Wandugu wapendwa. Ninaandika haya nikiwa nyumbani kwangu Dodoma. Najiandaa kwenda mahakamani kwa ajili ya uamuzi wa Mahakama Kuu juu ya kesi ya kutaka kuzuia Uchaguzi wa TLS. Ninawapa taarifa kwamba nimefuatwa nyumbani na askari wawili kutoka ofisi ya RPC Dodoma. Sijazungumza nao bado lakini ni wazi wana maagizo ya kunikamata na kunizuia kuja Arusha kwenye Uchaguzi wa TLS. Wameshindwa kuzuia uchaguzi wetu mahakamani. Sasa, kama kawaida ya serikali za kidikteta kila mahali, wanatumia mabavu ya kijeshi. Wito wangu kwenu mawakili wa Tanzania. Nendeni Arusha mkachague viongozi wa TLS watakaopigania haki za binadamu, utawala wa sheria na demokrasia. Msipofanya hivyo hakuna mtu yeyote, hata ninyi mawakili, atakayepona kwenye utawala wa aina hii. Kumbuka, kama Nimrod Mkono anaweza kufungiwa ofisi na TRA ni wakili gani mwingine aliye salama??? Kama wakili anaweza kukamatwa mahakamani kwa kufanya kazi yake ya uwakili, ni nani miongoni mwetu aliye salama??? Nendeni mkapige kura kukataa mfumo wa aina hii. Mimi naenda mahabusu, na pengine, gerezani. Nawaombeni kura zenu ili niweze kuwaongoza katika kipindi hiki kigumu. Hiki sio kipindi cha kuwa na viongozi wanaojipendekeza kwa wanaokandamiza haki za watu wetu na haki za mawakili wetu. Hiki ni kipindi cha kuwa na viongozi watakaopigania haki zenu na haki za watu wetu. Mnanifahamu. Nipeni jukumu hili la kuwaongoza kwenye giza hili nene. Msikubali kuyumbishwa. Na wachagueni pia Makamu wa Rais, Mweka Hazina wajumbe wa Governing Council watakaokuwa na msimamo kama wa kwangu. Nawatakieni kila la kheri. I'll think of you all wherever they'll take me to, wherever I'll be incarcerated. This too shall pass. The race of man shall rise again. It always has. Nimemwambia na mke wangu naye aende Arusha akapige kura. So, everybody to Arusha. Go vote your consciences. All the best.
Tundu Lissu
Wakati tukiwa na taaifa hii ndugu Godwin Ngwilimi  ameandika pia katika mitandao ya kijamii kama ninavyomnukuu hapa;
Nimeongea na RPC wa Dodoma afande L. B. Mambosasa ofisini kwake saa 5 na robo asubuhi hii kuhusu suala la mheshimiwa Tundu Lissu. Kwa maelezo yake, Tundu Lissu amekamatwa kwa maelekezo ya Kanda Maalum ya Polisi Dar es salaam ambako kuna shauri linalomkabili, na kwamba kuna tatizo la dhamana. Kwahiyo, wamemsafirisha kwenda Dar kwasababu hiyo.
Ni kweli, gari ya polisi iliyomchukua nyumbani kwake hadi kituo kikuu cha Polisi Dodoma, iliondoka hapo Mimi nikiwepo nasubiri kumuona RPC.
Vinginevyo, hivi sasa nipo mahakama kuu tukisubiri kusikiliza maamuzi ya mahakama katika mashauri aliyofungua Wakili Wasonga kuzuia uchaguzi wa TLS.
By Godwin Ngwilimi

1 comments:

  1. Maisha yangu Maajabu yanashangaza ushuhuda, Jinsi nimepata kisanduku chenye nguvu sana ambacho sasa ni pesa yangu mara mbili kutoka mia hadi elfu ya pesa ndani ya masaa 24, na pia jinsi nimerudisha mpenzi wangu wa zamani, sababu kuu niliwasiliana na Dk Lomi kwa msaada mimi kumrudisha mpenzi wangu wa zamani, basi ananisaidia ni nguvu kubwa ya kumrudisha mpenzi wangu wa zamani, na ananipenda na ananithamini sasa, basi mimi na Dr Lomi tukawa marafiki, baada ya mazungumzo kadhaa namuuliza ikiwa kuna njia anaweza kuniganga ili nipate pesa, hapo ndipo aliponiambia juu ya sanduku hili la uchawi, akaniambia kuna aina na saizi tofauti ya sanduku, aliniambia aina zote za sanduku, ningeweza kumudu ndogo tu ya sanduku, baada ya maombi muhimu anayofanya kwenye sanduku, ananipeleka kupitia huduma ya kujifungua, aliniambia niweke pesa ndani, niliweka ndani ya sanduku 100 euro baada ya masaa 24 nikagundua ilikuwa elfu 10 euro ndani, na nimekuwa nikitumia sanduku kwa miezi 7 sasa, mimi na mchumba wangu tunaishi maisha bora, ikiwa unahitaji b ack mpenzi wako au pesa spell wasiliana na Dr Lomi kwa barua pepe: lomiultimatetemple@gmail.com au WhatsApp namba +2349034287285 unaweza pia kumwandikia kupitia Jina la Mtumiaji la Snapchat: drlomi20 atakusaidia nje, asante kwa kusoma,

    Kwaheri Gerd Ulrich

    JibuFuta