Jumatano, Machi 29, 2017

EPL INAVYORUDI MWEZI APRILI

Baada ya kukaa pembeni kwa wiki mbili kupisha mechi za kimataifa, Manchester United wanarudi kilingeni Jumamosi Aprili 1 kwa kucheza nyumbani mechi ya ligi kuu England, dhidi ya West Bromwich Albion Uwanjani Old Trafford.
Mechi hiyo ni mwanzo wa mfululizo wa mechi 9 ambazo watazicheza mwezi Aprili na 7 kati ya hizo ni za EPL wakati 2 ni za UEFA EUROPA Ligi za robo fainali wakipambana na klabu ya Belgium Anderlecht.
Hivi sasa Man United wapo nafasi ya 5 kwenye ligi wakiwa na Pointi 52 kwa mechi 27 wakiwa nyuma ya timu ya 4 Liverpool kwa Pointi 2 lakini Liverpool wamecheza Mechi 2 zaidi yao wakati timu ya 3, Man City, wakiwa mbele yao kwa Pointi 5 lakini nao wamecheza mechi 1 zaidi yao.
Timu ya Pili ni Tottenham wenye pointi 59 kwa mechi 28 na vinara ni Chelsea wenye pointi 69 kwa mechi 28.

0 comments:

Chapisha Maoni