Jumatano, Machi 29, 2017

MABASI YA MWENDOKASI YAPATA AJALI DAR ES SALAAM

Mabasi mawili ya mwendokasi yamegongana leo asubuhi katika makutano ya Barabara ya Msimbazi na Morogoro jijini Dar es Salaam.
Katika ajali hiyo hakuna majeruhi wala mauti yaliyoripotiwa kutokea na inasemekana watu wote wametoka salama isipokuwa uharibifu wa taa zakuongozea magari katika eneo hilo na uharibifu mkubwa kwa mabasi yenyewe.
Aidha chanzo cha ajali hiyo hakijajulikana bado hadi pale mamlaka husika itakapotoa taarifa kuhusu ajali hiyo.

0 comments:

Chapisha Maoni