Alhamisi, Machi 30, 2017

AJIKATA UUME WAKE NA KUMPATIA MBWA, KISA?

Mwanaume kutoka Naivasha nchini Kenya ameushangaza ulimwengu baada ya kuamua kuukata uume wake kwa madai kwamba hauna faida yoyote kwake nakumwachia mbwa kiungo hicho kama chakula. 
Taarifa zilizopatikana kutoka nchini Kenya zinaeleza kuwa tukio hilo limetokea siku ya alhamisi ambapo jamaa huyo alichukua mkasi na kisha kujikata uume wake na kisha kumalizia kukata kiungo hicho kwa kisu kilichokuwa karibu nae.
Baada ya mwanamume huyo kukata uume wake alisikika akipiga mayowe kutoka chumbani kwake katika nyumba anayoishi na kufanya watu waliokuwa wapita njia kuita polisi kwaajili ya kumpatia msaada huyo bwana.
Kutokana na maumivu aliyokuwa nayo mhanga na kutokana na kutokwa na damu nyingi bwana huyo alifikishwa katika hospitali ya Naivasha ili kupatiwa huduma zaidi ambapo shuhuda Joseph Chege kuwa walimkuta huyo bwana akiwa nusu utupu na jeraha kubwa.
Mkenya huyo alipoulizwa baada ya kuingizwa katika chumba cha upasuaji akaeleza kuwa tatizo kubwa lililomfanya ajikate uume ni kutokana kile alichodai kuwa kiungo hicho muhimu kwa mwanaume kutomsaidia katika maisha yake.
Inadaiwa kuwa imewahi kusikika mitaani kwamba huyo bwana si ridhiki na hawezi kushirikiana na mwanamke wa namna yoyote.

0 comments:

Chapisha Maoni