Jumamosi, Februari 25, 2017

VIDEO YA MAGOLI YOTE MATATU KATIKA MECHI YA SIMBA VS YANGA LEO TAIFA

Klabu ya soka ya Simbaimeichapa Yanga 2-1 uwanja wa Taifa Temeke, Dar es Salaam na kuendelea kukaa kileleni mwa ligi kuu soka Tanzania bara msimu wa 2016-2017.

Ikiwa ni mechi ya pili kwa msimu huu kukutana watani hao wa jadi wenyeji wa Kariakoo jijini Dar, huku ikiwa ni mchezo wa raundi ya pili, winga Ramadhani Kichuya anaifanya Simba kuzima ubishi na tambo za mahasimu wao Yanga baada ya kufunga goli la pili dk 81 baada ya lile la kusawazisha lililofungwa na Laudit Mavugo dk 66. Hii ni baada ya bao la Msuva alilofunga kwa mkwaju wa penati dk 5 na kuifanya Yanga kuongoza mpaka dk ya 65.
Video ya magoli yote matatu katika mechi hiyo hii hapa:

0 comments:

Chapisha Maoni