Alhamisi, Februari 23, 2017

UPINZANI KENYA KUSIMAMISHA MGOMBEA URAIS MMOJA KATIKA UCHAGUZI MKUU

Viongozi wa vyama vikubwa vya upinzani vya Kenya vyakubaliana kuweka mgombea mmoja wa urais
Viongozi wa vyama vikubwa vya upinzani vya Kenya wamekubaliana kuweka mgombea mmoja wa urais, na kutoa mwito kwa vyama vyote kuwa makini kuhakikisha kuwa hakuna njama za kufanya udanganyifu kwenye uchaguzi.
Hata hivyo muungano mpya mkubwa wa upinzani unaojulikana kama NASA haukutaja jina la mgombea wake, kuwa wanasheria na wataalamu wake wamekuwa wakiandaa makubaliano kuhusu namna ya kugawana madaraka.
Aliyekuwa makamu wa Rais wa Kenya Bw. Kalonzo Musyoka amesema muungano mpya wa wapinzani una nguvu mpya, na unaoongozwa kwa kanuni ya nia njema. Muungano huo unaundwa na vyama vya ODM kinachoongozwa na Raila Odinga, FORD-Kenya kinachoongozwa na Bw Moses Wetangula, ANC kinachoongozwa na Bw Musalia Mudavadi na WIPER kinachoongozwa na Bw Musyoka

0 comments:

Chapisha Maoni