Jumamosi, Februari 25, 2017

UMEWAHI WAZA NI KIASI GANI CHA MAJI KINAWEZA KULIZIMA JUA?

Kwa kawaida tunafikiri jua ni kama mpira mkubwa wa moto, ambao unatupatia mwanga na joto. Sasa kuna swali moja la ajabu, tukitaka kuzima jua, tutafanyaje?
Labda watu wengi wanaweza kujibu tukiwa na maji mengi ya kutosha, tutaweza kuyamwaga kwenye jua. Je, hatua hii kweli itafanya kazi?
Jua si mpira wa moto wa kawaida. Nishati ya jua inatokana na uunganishaji nyuklia (nuclear fusion), ambao ni mchakato wa atomu za Hydrogen kuunganishwa pamoja na kuunda atomu ya Helium katika mazingira yenye shinikizo kubwa. Inakadiriwa kuwa shinikizo katika kiini cha jua ni mara laki 3.33 ya shinikizo la hewa ya duniani, na joto la huko ni nyuzi milioni 15 sentigredi.
Je tukipata maji mengi yenye ukubwa sawa na jua, kugandisha maji hayo na kutupa barafu kwenye jua, tutaweza kuzima jua? Jibu ni kwamba hatutafanikiwa, kwani barafu ikikaribia jua, itavukizwa kutokana na joto kali.
Lakini ukifanikiwa kuingiza mvuke mwingi sana ndani ya jua, jua litazimwa? Jibu bado ni hapana, kwa sababu jua lina joto kali, mvuke utagawanyika na kuwa Hydrogen na Oxygen. Na jambo baya zaidi ni kwamba Hydrogen ni malighafi ya mchakato wa uunganishaji nyuklia, hivyo jua litapata nishati nyingi zaidi, ukubwa wa jua utakuwa mara 1.3 ya hivi sasa, na litawaka zaidi na kuwa moto zaidi. Wakati huo joto la duniani litakuwa mara 6 ya hivi sasa, na viumbe vyote vitakufa.

0 comments:

Chapisha Maoni