Jumamosi, Februari 25, 2017

'MAMA ONGEA NA MWANAO' KUWEKA HADHARANI MADAI YAO DHIDI YA CCM, KUKANUSHA ALICHOKIZUNGUMZA STEVE NYERERE

Kundi la MAMA ONGEA NA MWANAO katika kampeni 2015

Unaikumbuka timu ya MAMA ONGEA NA MWANAO? Hii ilikuwa maarufu sana mwaka juzi 2015 kuelekea uchaguzi mkuu wa oktoba25 mwaka huo, ambapo ilikuwa ikifanya kampeni ya nguvu kuhakikisha CCM inapata ushindi mkuu katika uchaguzi huo, walifanikiwa!
Jambo ambalo linaleta mzozo mpaka sasa ni suala la malipo yao, ambapo timu hiyo iliyokuwa na wasanii na mastaa kibao nchini imedai kuwa imeambulia patupu katika malipo.
Jana msanii wa movie Tanzania na mchekeshaji maarufu Steven Mengele maarufu kama Steve Nyerere alidai kuwa hakuna mtu yeyote kutoka katika timu hiyo anaeidai CCM baada ya shughuli za kampeni, Steve aliyazungumza hayo wakati akiongelea sakata la Wema Sepetu na Dawa za kulevya.
Steve Nyerere akizungumza na waandishi wa habari jana

Utakumbuka siku chache zilizopita ilivuja sauti akisikika Steve akizungumza na Mama Sepetu na kuwataja baadhi ya viongozi wakubwa nchini kuwa alizungumza nao ili kumnusuru Wema na ishu iliyokuwa imemtia mbaroni kuhusu dawa za kulevya.

Kubwa kwa sasa ni kwamba timu hiyo ya MAMA ONGEA NA MWANAO imepanga kuzungumza na waandishi wa habari ili kukanusha kile kilichozungumzwa na Steve Nyerere kuwa tayari wamelipwa pesa zao jambo ambalo wanadai sio la kweli.

Wanasema wanaidai CCM mamilioni ya fedha na wanataraji kuweka madai yao hadharani zikiwemo documents za malipo, mkataba na vielelezo vingine.

VIDEO WAKATI STEVE NYERERE AKIZUNGUMZA NA WANAHABARI JANA HII HAPA:

0 comments:

Chapisha Maoni