Ijumaa, Februari 24, 2017

KOCHA CLAUDIO RANIEL WA LECEISTER CITY ATIMULIWA

Menenja Claudio Ranieri ametimuliwa na klabu ya Leicester City, miezi tisa tu baada ya kuiongoza klabu hiyo kubeba kombe kwenye ligi ya Premier.
Leicester wana pointi moja tu kushuka daraja wakiwa wamesaliwa na mechi 13. Kwa mujibu wa taarifa, bodi imesema inaona mabadiliko ya uongozi ni muhimu kwa maslahi ya klabu. Ranieri mwenye miaka 65, ameiongoza Leicester kubeba taji licha ya kuwa na hali mbaya mwanzoni mwa kampeni zake. 
Hata hivyo habari ya kufukuzwa kocha huyo imewasikitisha wengi.
Kutimuliwa kwake kumekuja chini ya saa 24 baada ya kufungwa 2-1 na timu ya Hispania Sevilla katika mzunguko wa kwanza wa ligi ya mabingwa. Leicester wanaweza kuwa mabingwa wa kwanza watetezi kushushwa daraja tangu 1938. 
Mapema mwaka huu Leicester ilimpa sapoti Muitaliana huyo aliyeteuliwa kuwa meneja July 2015 na kusaini mkataba mpya wa miaka minne Agosti 2016. 
Meneja msaidizi Craig Shakespeare na kocha Mike Stowell watasimamia kikosi hadi atakapopatikana meneja mpya.

0 comments:

Chapisha Maoni