Tetemeko la ardhi ya ukubwa wa 5.7 kwenye vipimo vya Richter limekumba maeneo ya Ziwa Tanganyika usiku wa kuamkia leo.
Tetemeko
hilo lilitikisa maeneo ya kaskazini mwa Zambia na mitetemeko hiyo
ikasikika maeneo ya kusini magharibi mwa Tanzania, hasa eneo la Rukwa.
Kitovu
cha tetemeko hilo, kwa mujibu wa Shirika la Utafiti wa Jiolojia la
Marekani, kilikuwa kilomita 10 chini ya ardhi umbali wa kilomita 45
mashariki mwa mji wa Kaputa nchini Zambia.
Mji huo unapatikana katika mpaka wa nchi hiyo na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.
Tetemeko hilo lilitokea mwendo wa saa tisa na dakika thelathini na mbili usiku (0032 GMT).
Tetemeko
la ardhi la ukubwa kama huo huchukuliwa kuwa la kadiri lakini wataalamu
wanasema kutokana na hali kwamba kitovu chake chakikuwa chini sana
ndani ya ardhi, huenda hilo lilisababisha mitikisiko kuwa mikubwa.
Desemba mwaka 2005, tetemeko kubwa la ardhi lilitokea eneo la Ziwa Tanganyika.
Tetemeko hilo la nguvu ya 6.8 lilitikisa majumba katika miji maeneo ya Afrika mashariki na kati.
0 comments:
Chapisha Maoni