Jumamosi, Februari 25, 2017

FAIDA KUU YA KUTENGANISHA TAKA NA KUZIRUDISHA KATIKA MATUMIZI

Maarifa ya nchi mbalimbali yanaonesha kuwa kugawanya aina tofauti za takataka kunasaidia mzunguko wa rasilimali na kutatua tatizo la uchafuzi wa takataka mijini.
Watu wanapotaja mji wa New York Marekani hufikiri huu ni mji wa kisasa wa kuvutia. Lakini kabla ya mwishoni mwa karne ya 19, New York ni mmoja ya miji michafu zaidi duniani. Wakati huo takataka zenye harufu mbaya na nzi zilionekana kote mjini. Mwaka 1895, mhandisi wa usafi Bw. George E. Waring alianzisha mfumo wa kwanza wa kugawanya aina tofauti za takataka ili kuzitumia tena mjini humo, na kutoa mwito kwa wakazi wote kusafisha barabara. Kwa mujibu wa sheria zilizotungwa mwaka 1989, wakazi wa New York wanatakiwa kugawanya takataka kabla ya kutupa. Katika miaka ya hivi karibuni, mji huo unajaribu kukusanya takataka za vyakula ili kuzitumia kuzalisha gesi za kinyesi na mbolea.
Mji wa Tokyo nchini Japan wenye idadi kubwa ya wakazi pia uliwahi kusumbuliwa na uchafuzi wa takataka. Baada ya kufanya juhudi kwa muda mrefu, mazingira ya mji huo yameboreka kwa kiasi kikubwa. Kutupa takataka si jambo rahisi, kwa mfano, ukitaka kutupa pakiti ya sigara, unatakiwa kuzigawanya katika sehemu tatu, yaani mfuko wa plastiki ni takataka ya plastiki, pakiti ya karatasi ni takataka inayoweza kuteketezwa, na karatasi ya kufungia ya aluminum ni takataka ya metali.

0 comments:

Chapisha Maoni