Jeshi la Nigeria limeokoa takriban watu 11,595 waliokuwa wameshikwa
mateka na kundi la wanamgambo wa Boko Haram katika kipindi cha mwezi
moja uliopita.
Kulingana na taarifa uliotolewa na jeshi kupitia
msemaji wake Sani Usman, watu hao waliokolewa kwenye operesheni
zilizofanywa kaskazini mashariki mwa nchi kati ya mwezi Februari 26 na
Mechi 31 huku wengine wakikombolewa na maafisa wa usalama wa Cameroon.
Boko Haram wameua maelfu ya watu tangu kundi hilo lilipoanza
mashambulizi kaskazini mashariki mwa Nigeria mwaka wa 2009. Ingawa jeshi
la Nigeria limekomboa maeneo mbali mbali yaliyokuwa chini ya udhibiti
wa Boko Haram, kundi hilo lingali lina uwezo wa kutekeleza mashambulizi
hatari nchini humo.
0 comments:
Chapisha Maoni