Serikali ya Tanzania jana (Jumatano) ilitangaza bajeti ya dola
bilioni 13 katika makadirio yake ya fedha ya mwaka 2016/2017 itakayoanza
mwezi wa Julai.
Bajeti hiyo inanuia kupunguza kwa kikubwa
utegemezi wa wafadhili, alisema waziri wa fedha Philip Mpango huku
akiongeza kuwa wafadhili watagharimia dola bilioni 1.5 pekee ya bajeti
hiyo. Mpango alisema kuwa miradi nyingi ya maendeleo nchini humo
imesimama kwa sababu ya wafadhili kutotoa ama kuchelewa kutoa fedha
walizoahidi. “Serikali inafanya
mazungumzo na wafadhili ili kuweka taratibu za kuaminika na kuhakikisha
kuwa wafadhili wanatimiza ahadi wanazotoa,” Mpango aliambia waandishi wa
habari mjini Dar es Salaam.
Waziri huyo alisema kuwa serikali ya Tanzania sasa inajitahidi
kujitegemea kwa njia ya ukusanyaji wa ushuru ili kuepukana na masharti
yanayotolewa na wafadhili. “Tunawaonya vikali wafanyibiashara wanaokwepa
kulipa ushuru na wafanyikazi wa umma wanaotumia vibaya pesa za umma
kuwa tutawachukulia hatua ya kisheria,” alionya waziri Mpango.
Katika hotuba yake bungeni mwezi Februari mwaka jana, Mpango aliambia
wabunge kuwa serikali inanuia kupunguza utegemezi wa wafadhili kutoka
asilimia 6.4 hadi asilimia tatu. Aliongeza kuwa upungufu huo utajazwa
kwa kuongeza kodi inayotozwa juu ya mapato na asilimia 15 na kupunguza
matumizi mabaya ya pesa za umma.
0 comments:
Chapisha Maoni