Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia
na Ufundi inakanusha taarifa inayosambazwa katika mitandao ya kijamii
yenye kichwa cha habari “NDALICHAKO NA WALIMU TZ”.
Taarifa hiyo inadai kuwa Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi Prof. Joyce Ndalichako amesema kuwa walimu wanaandaliwa sare watakazo vaa wakati wa kazi.
Tunapenda kuufahamisha umma kuwa Taarifa hizi si za kweli. Aidha, Wizara inawataka watu wanaoeneza taarifa za kizushi za aina hii waache kufanya hivyo ili kuepusha usumbufu unaojitokeza.
Hatua za kisheria zitachukuliwa kwa watakaobainika kuanzisha na kueneza uzushi huu.
IMETOLEWA NA
KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI
07/04/2016

0 comments:
Chapisha Maoni