Ukatili wa majumbani unaua mwanamke moja kila baada ya masaa 30 nchini Argentina, na matukio inaendelea kupanda, kulingana na ripoti iliyotolewa Alhamisi.
Ripoti hiyo "Femicide Watch" iliyochapishwa na shirika lisilo la kiserikali La Casa del Encuentro, inaonyesha kwamba wanawake 286 waliuawa na unyanyasaji wa kijinsia mwaka 2015, kutoka 277 mwaka 2014 na kuacha watoto 214 yatima.
Kati yao, 121 waliuawa na waume wao, au marafiki wa kiume wa sasa au wa zamani.
0 comments:
Chapisha Maoni