Utafiti mpya uliofanywa nchini Japani umeonesha kuwa, upimaji wa idadi
ya protini maalumu katika damu unaweza kukadiri hatari ya kupata ugonjwa
wa Alzheimer. Watafiti wanaona kuwa ugunduzi huo utasaidia kutambua
ugonjwa huo mapema.
Ugonjwa wa Alzheimer unadhaniwa kuhusiana na protini ya amyloid B. Protini hiyo inaweza kuharibu seli za ubongo na kuathiri sehemu yenye uwezo wa kukumbuka na kutambua. Kiafya, protini ya amyloid β inaweza kuondolewa kwenye ubongo kupitia damu. Katika mchakato huo, protini nyingine tatu zitatoa mchango mkubwa.
Watafiti walichambua takwimu husika za wazee wa wilaya ya Ibaraki na mji wa Kyoto nchini Japani, wakagundua kuwa kwa kulinganishwa na wazee wenye afya, katika damu ya wazee wenye tatizo la ufahamu idadi ya protini hizi tatu inapungua.
Kiwango cha usahihi cha upimaji huo wa damu kimefikia asilimia 80 hivi.

0 comments:
Chapisha Maoni