Serikali imesema itakichukua kiwanda cha viatu cha Bora na vingine ambavyo vimeshindwa kutekeleza makubaliano ya kuzalisha kwa tija, kulipa kodi na kutoa kipaumbele cha ajira kwa wazawa ifikapo Septemba mwaka huu. Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mheshimiwa CHARLES MWINJAGE amesema serikali inatambua mchango wa sekta binafsi katika kuchangia pato la taifa na ukuaji wa uchumi na kusisitiza msimamo wa serikali ni kufufua na kuongeza viwanda ili kuongeza ajira ma kukuza uchumi.
0 comments:
Chapisha Maoni