Tanzania inatafuta msaada wa dola bilioni 10 kutoka kwa wafadhili mbali mbali nchini India kufikia malengo yake ya maendeleo ikiwemo ujenzi wa miundombinu, hii ni kwa mujibu wa ripoti iliyotolewa na shirikisho la viwanda nchini India (CII).
Kulingana na ripoti hiyo, fedha hizo zitatolewa na serikali ya India kwa ushirikiano na benki ya Exim ya India pamoja na wawekezaji nchini humo. Aidha ripoti hiyo inasema kuwa shirika linalosimamia makazi nchini Tanzania, National Housing Corporation (NHC) ndilo litakalopokea kiasi kikubwa zaidi cha fedha hizo. NHC itapata dola bilioni 6.2 ikifuatwa na mamlaka ya bandari (Tanzania Ports of Authority) itakayopokea dola milioni 598.
Tanzania pia imetoa ombi la dola bilioni 1.08 kutoka India kufadhili miradi mbali mbali ya ujenzi wa barabara, huku barabara ya Dar es Salaam-Chalinze-Morogoro ikitengewa dola milioni 519. Taifa hilo la Afrika mashariki pia limetoa ombi la dola bilioni 1.3 kufadhili miradi ya nishati na dola milioni 9.1 kufadhili miradi ya kilimo.
0 comments:
Chapisha Maoni