Jeshi la Polisi wilayani Kibondo mkoani Kigoma limeteketeza zaidi ya tani moja na nusu ya bangi iliyokuwa imepandwa katika shamaba la ukubwa wa hekari mbili katika kijiji cha Kagoti kata ya Misezero wilayani humo.
Mkuu wa wilaya ya Kibondo Ruth Msafiri amesema, walipata taarifa za kuwepo shamba la bangi katika kijiji hicho hali iliyowalazimu kufika kijijini hapo alfajiri na kufanya ukaguzi ambao ulibaini shamba hilo likiwa limechanganywa na mazao mengine na kwamba wataendelea kuchukua hatua dhidi ya wananchi ambao wameamua kulima bangi badala ya mazao yanayokubalika.
Kwa upande wake mkuu wa polisi wilaya ya Kibondo mkaguzi msaidizi wa polisi Maiko Joshua amesema pamoja na bangi iliyokutwa shambani, baada ya upekuzi katika nyumba ya watuhumiwa wamekuta kilo moja ya bangi kavu na kwamba watuhumiwa watafikishwa mahakamani wiki hii.
0 comments:
Chapisha Maoni