Ijumaa, Machi 11, 2016

MSHUKUWA WA UGAIDI AHUKUMIWA KIFO KENYA

Mahakama kuu mjini Mombasa, Kenya imetoa hukumu ya kifo kwa mshukiwa wa ugaidi, Thabit Yahya, aliyeshtakiwa miaka minne iliyopita kwa kosa la kulipua mgahawa mmoja ambapo mtu mmoja aliuawa na wengine wengi kujeruhiwa.
Shambulizi hilo lililotokea mwezi Mei mwaka wa 2012 wakati wa usiku katika mgahawa uliojulikana kama Bella Vista ambapo watu wengi walijeruhiwa na mlinda mlango mmoja kuuawa, wakati washambuliaji walipotumia maguruneti kutekeleza kitendo hicho.
Serikali ya Kenya sasa inaonekana kutekeleza sheria mpya ya kuwaadhibu.
magaidi, kama ilivyopitishwa katika marekebisho ya sheria kuhusu usalama wa taifa la Kenya.

0 comments:

Chapisha Maoni