Utafiti mpya uliofanywa nchini Marekani umegundua kuwa, kutembea katika
mazingira ya kimaumbile kunasaidia afya ya kisaikolojia na kupunguza
hatari ya kupata mfadhaiko.
Kufutatia maendeleo ya utandawazi wa miji, kiwango cha maradhi ya kisaikolojia ukiwemo mfadhaiko kinaongezeka kidhahiri. Watafiti wa chuo kikuu cha Stanford walifanya utafiti uliolenga kutafuta uhusiano kati ya kugusa mazingira ya kimaumbile na maradhi ya kisaikolojia.
Watafiti waligawa makundi mawili ya watu na kuwataka kutembea kwa saa moja na nusu. Kundi la kwanza walitembea katika sehemu ya misitu, na kundi lingine walitembea katika barabara za miji.
Baada ya matembezi hayo, watafiti walipima moyo na ubongo wao na kugundua kuwa, sehemu moja ya ubongo wa watu waliotembea katika mazingira ya kimaumbile ilitulia sana, ambayo inadhaniwa kuhusiana na mfadhaiko.
Watafiti wameshauri kuwa katika mchakato wa ujenzi wa miji, wapangaji wanatakiwa kutambua umuhimu wa mazingira ya kimaumbile.

0 comments:
Chapisha Maoni