Alhamisi, Machi 31, 2016

MKOJO UNAVYOTUMIKA KUPIMA SARATANI

Saratani ya matiti ni uvimbe unaoonekana zaidi kati ya wanawake, na jinsi ya kutambua saratani hiyo kwa urahisi zaidi ni utafiti muhimu unaofanyika katika miaka ya hivi karibuni. Watafiti wa Ujerumani wamesema, wamebuni njia ya kutambua saratani ya matiti kwa kupima kiwango cha miRNA katika mkojo, ambayo kiwango cha sahihi kimezidi asilimia 90.
Utafiti mwingi umethibitisha kuwa miRNA ni muhimu sana katika mchakato wa ongezeko na uhamiaji wa seli za saratani ya matiti. Watafiti wa chuo cha matibabu cha chuo kikuu cha Freiburg cha Ujerumani wamesema, wamepima mkojo wa wagonjwa 24 wa saratani ya matiti na wanawake wengine 24 wa kawaida, na kuchambua kiwango cha miRNA kwenye mkojo wao.
Matokeo yameonesha kuwa katika mkojo wa wagonjwa wa saratani ya wamatiti, kiwango cha miRNA ni cha juu zaidi. Watafiti wamesema, upimaji huo ni rahisi zaidi, ambao kiwango cha usahihi kimefikia asilimia 91. Upimaji huo unatarajiwa kutumiwa katika kutambua saratani hiyo katika kipindi cha mwanzo.

0 comments:

Chapisha Maoni