Watafiti wa Uingereza wamesema, kama wanawake watapata mfadhaiko katika kipindi cha ujauzito, kiwango cha kupata mfadhaiko cha watoto wao pia kitaongezeka kwa kiasi kikubwa.
Watafiti wa chuo kikuu cha London, Uingereza walichunguza na kufuatilia hali za afya za wajawazito 103 na watoto wao ambao walizaliwa mwaka 1987 hivi.
Matokeo yameonesha kuwa kati ya wajawazito hao, wanawake 35 walipata mfadhaiko wa uja uzito, na asilimia 57 ya watoto wao walipata mfadhaiko baada ya kuwa watu wazima. Kwa wajawazito wale wasiopata mfadhaiko, kiwango cha mfadhaiko cha watoto wao ni asilimia 28 tu.
Watafiti wameongeza kuwa mfadhaiko baada ya uzazi wa wanawake hauna uhusiano mkubwa na mfadhaiko wa watoto.
Utafiti wa awali ulionesha kuwa katika kipindi cha ujauzito, mfadhaiko wa wanawake utasababisha homoni ya shinikizo kuongezeka na kuathiri ukuaji wa ubongo wa watoto.
Watafiti wameshauri kuwa, kama wajawazito wataonesha dalili za mfadhaiko watatakiwa kupatiwa tiba mapema, ili kupunguza athari mbaya kwa watoto wao.
0 comments:
Chapisha Maoni