Jumamosi, Machi 12, 2016

KAGAME WA RWANDA KATIKA NYAYO ZA MAGUFULI, AKEMEA SAFARI ZA NJE

Rais wa Rwanda Paul Kagame amesema hatavumilia matumizi holela ya fedha za walipa kodi nchini mwake, amesema anakubaliana na hatua anazochukua rais wa Tanzania, Dkt. Magufuli.
Amesema hayo akiwahutubia viongozi nchini mwake waliohudhuria semina maalum ya kujitafakari.
Amesema hatavumilia safari zisizo na tija, na atazipunguza kwa kiasi kikubwa.
Amesema fedha za safari zinatakiwa kutumika kwa ajili matatizo ya wananchi wake.
Pia amegusia mkutano wa wakuu wa nchi za Afrika Mashariki uliofanyika Arusha.

0 comments:

Chapisha Maoni