Wafungwa 6 wa kike wanaoshikiliwa katika jela ya mji wa New York
nchini Marekani wamewasilisha mashtaka ya kufanyiwa ukatili wa kijinsia
na maafisa wa jela hiyo.
Wahanga hao wa unyanyasaji wa kingono katika jela ya New York
wamewasilisha mashtaka yao katika Mahakama ya Federali ya Manhattan
wakisema kuwa maafisa wa jela hiyo wamekuwa wakifumbia jicho unyanyasaji
wa kingono wanaofanyika katika jela hiyo. Wamesema kuwa kila mara
wanapowasilisha mashtaka na kufanyiwa ukatili wa kingono wamekuwa
wakikabiliwa na mashinikizo makubwa zaidi.
Wiki iliyopita pia afisa wa polisi ya jimbo la Oklahoma nchini
Marekani alihukumiwa kifungo cha miaka 263 ambacho ndicho kifungo cha
juu zaidi nchini humo baada ya kupatikana na hatia ya kubaka wanawake
kadhaa akiwa kazini.
Ripoti ya kila mwaka ya shirika la kutetea haki za binadamu la
Amnesty International pia imelalamikia ukiukwaki wa haki za binadamu
unaofanyika nchini Marekani kama mateso yanayofanywa na maafisa wa
shirika la ujasusi la nchi hiyo CIA dhidi ya mahabusu waliokamatwa
kinyume cha sheria na utumiaji wa mabavu wa polisi ya nchi hiyo.
0 comments:
Chapisha Maoni