Viongozi wa nchi za Afrika Mashariki watakutana Arusha, Tanzania
Jumatano ijayo kujadili upigaji marufuku uingizaji wa nguo zilizotumika
au mitumba, magari yaliyotumika na bidhaa za ngozi kutoka nje ya eneo
eneo hilo.
Taarifa iliyotolewa na jumuiya hiyo imesema itatafakari pendekezo
la kuanzishwa viwanda vya utengenezaji magari na hivyo kupungua
uingizaji magari yaliyotumika sambamba na kuimarisha viwanda vya nguo na
ngozi katika nchi wanachama.
Kikao hicho cha Machi 2 pia kitajadili njia za kuanzisha Shirikisho
la Kisiasa la Jumuiya ya Afrika Mashariki. Halikadhalika viongozi wa
kanda hiyo watazindua paspoti za kielektroniki ambazo zitatumika
kurahisisha usafiri kwa wananchi wa eneo hilo.
Watu wa Afrika Mashariki wamekuwa wakisubiri pasi hiyo kwa muda mrefu
na hivyo kuzinduliwa kwake ni hatua muhimu katika kuimarisha
ushirikiano wa nchi tano wanachama ambazo ni Burundi, Kenya, Rwanda,
Tanzania na Uganda.
Katika kikao hicho, wakuu wa EAC watajadili ombi la Sudan Kusini na Somalia kutaka kujiunga na jumuiya hiyo.
0 comments:
Chapisha Maoni