Watu wengi wanachukua msimamo ambao kukaa kwa muda mrefu kunaweza kuharibu afya na hata kusababisha vifo. Lakini watafiti wa Uingereza wamesema, kitendo chenyewe cha kukaa kwa muda mrefu hakina uhusiano na hatari ya kusababisha kifo.
Watafiti wa chuo kikuu cha Exeter katika miaka 16 iliyopita walifuatilia watu zaidi ya elfu 5, na kuweka kumbukumbu kuhusu muda wao wa kukaa, kutembea na mazoezi mengine pamoja na tabia ya kukaa ofisini na nyumbani. Matokeo yanaonesha kuwa kitendo cha kukaa kwa muda mrefu hakitaleta athari yoyote kwa afya.
Watafiti wanafafanua kuwa kinachoweza kusababisha vifo ni ukosefu wa mazoezi, wala sio kukaa kwa muda mrefu. Utafiti unaonesha kuwa kupunguza muda wa kukaa hakuna umuhimu mkubwa katika kupunguza hatari ya vifo.
0 comments:
Chapisha Maoni