Jumapili, Februari 21, 2016

KIFO CHA MALCOLM X SIKU KAMA YA LEO

Siku kama ya leo 51 iliyopita, Malcolm X, Mmarekani mweusi aliuawa baada ya kushambuliwa na magaidi nchini humo. Malcolm X alizaliwa mwaka 1925, na wakati alipokuwa kwenye rika la ujana alifahamiana na makundi ya vijana wa Kiislamu na hatimaye kusilimu. Itikadi ya mwanaharakati huyo wa Kiislamu iliwachukiza watawala wa Marekani na makundi ya ubaguzi wa rangi nchini Marekani. Malcolm X aliuawa akihutubia mkutano. Alikuwa akisisitiza mara kwa mara kuwa, Wamarekani weusi ambao wanakandamizwa na kubaguliwa na serikali ya Marekani wanaweza kujipatia uhuru na uadilifu chini ya mwavuli wa utawala wa Kiislamu.

0 comments:

Chapisha Maoni