Alhamisi, Februari 25, 2016

UGONJWA USIOFAHAMIKA WAENDELEA KUUA WANAIJERIA

Watu 13 wamethibitishwa kufariki tangu wiki iliyopita kutokana na maradhi yasiyojulikana jijini Abuja, Nigeria, afisa mmoja wa afya amesema.
Ugonjwa huo ambao unashukiwa kuwa aina ya homa ya matumbo ulizuka Februari 18 katika kijiji cha Saburi ndani ya manispaa ya Abuja. Waathirika wa ugonjwa huo wanasemekana kuonyesha dalili za maumivu ya tumbo na homa kali kisha wanahara damu hadi kufa. Tayari sampuli za damu zimechukuliwa kutoka kwa walioathiriwa na kupelekwa kwenye mahabara kwa utafiti zaidi. Hakuna muathiriwa ambaye ameponea baada ya kuonyesha dalili hizo, isipokuwa mtoto mmoja wa miaka mitano.

0 comments:

Chapisha Maoni