Alhamisi, Februari 25, 2016

UCHAFU WA MDOMO HUENDA UTASABABISHA KUVUJA DAMU KWENYE UBONGO

Utafiti mpya uliofanywa nchini Japani unaonesha kuwa, streptococcus inayoweza kusababisha karisi ina uhusiano na kuvuja damu kwenye ubongo. Streptococcus hiyo inaweza kuzuia damu kutoka mwilini. Watafiti wanaona kuwa ugunduzi huo utasaidia kutafuta njia mpya ya kuzuia kuvuja damu kwenye ubongo. Pia wanaona kuwa, streptococcus inaweza kuingia kwenye mishipa ya damu ya mdomoni, kisha kufuata mzunguko wa damu kufikia mishipa ya damu ya ubongo na hatimaye kusababisha kuvuja damu kwenye ubongo.
Wataalam hao wamesema, kuvuja damu kwenye ubongo ni aina moja ya kiharusi, ulaji wa chumvi nyingi pia ni chanzo kingine. Lakini utafiti huo umeonesha usafi wa mdomo na matibabu ya meno ni muhimu kwa kinga ya kuvuja damu kweny ubongo.

0 comments:

Chapisha Maoni