Serikali imeagiza wakandarasi wote waliositisha ujenzi wa miundombinu mbalimbali nchini kuanza kazi mara moja baada ya kufanikiwa kuwalipa madeni yao zaidi ya shillingi billion 400 kati ya deni la trilion 1.2 lililoachwa na serikali ya awamu ya nne.
Agizo hilo limetolewa na waziri wa ujenzi, uchukuzi na mawasiliano Prof, Makame Mbarawa mkoani Morogoro ambapo amesema katika kipindi cha miezi mitatu serikali ya awamu ya tano imefanikiwa kuwalipa wakandarasi kiasi cha shiling bilion 400 ambapo mpaka kufikia mwezi juni mwaka huu wakandarasi wote watakuwa wamelipwa fedha zao, huku agizo hilo likienda sambamba na kumtaka mkandarasi wa barabara ya Dakawa, Turiani kuendelea na ujenzi wa barabara.
Aidha katika hatua nyingine waziri Mbarawa akiwa katika ziara yake mkoani Morogoro akiambatana na naibu wazi wake Mhandisi Edwin Ngonyani wametembelea katika karakana ya TRL ambako inafanyika na kuzungumza na wafanyakazi ambapo alikuwa mbogo kwa kuwaonya wale wote watakao bainika kutengeneza ajali za treni kwa makudi serikali haitawavumilia, watafukuzwa kazi sambamba na kufikishwa mahakani.
Nao wafanyakazi wa shirika hilo wamotoa malalamiko yao kwa waziri huyo wakidai serikali kuwasahau kwa kuimarisha miundo mbinu ikiwa ni pamoja na stahiki zao na kusababisha kuishi maisha ya kiumaskini.
Waziri Mbarawa katika ziara yake yakukagua miradi mbalimbali alitembelea barabara ya Magole Turiani, kitio cha mawasiliano cha Halotel, karakana ya reli pamoja na kituo cha mizani cha Mikese mkoani Morogoro.
0 comments:
Chapisha Maoni