Kufuatia Tangazo kwa Umma lilitolewa kwenye vyombo vya Habari na
kuchapishwa kwenye Magazeti, Uongozi wa Chama cha Wamiliki na
Waendeshaji wa Vituo vya Mafuta Nchini (TAPSOA) ulikutana na Kaimu
Kamishna Mkuu na kufanya majadiliano ya msingi kuhusu matumizi ya EFD na
kufunga Mashine za EFD Maalum katika vituo vya mafuta kwa ajili ya
kutolea risiti za mauzo. Makubaliano ya pamoja kutokana na majadiliano
ni kwamba, agizo la Kaimu Kamishna Mkuu liendelee kutekelezwa katika
utaratibu ufuatao;
(a) Wamiliki wote wenye vituo vya mafuta walio
katika kundi la Makampuni makubwa wanaoagiza mafuta na kutumia Mawakala
kusambaza/kuuza mafuta kwa wateja (CODO) wakamilishe kufunga Mashine za
EFD katika vituo vyao vyote Nchini kama ilivyokubalika katika kikao
hicho (yaani kufikia tarehe 15 Machi 2016).
(b) Wamiliki wote
wenye vituo vya mafuta walio katika kundi la Makampuni wanaoagiza mafuta
na kusambaza/ kuuza mafuta kwa wateja wao wenyewe (COCO) walioanza na
wanaofunga Mashine za EFD kwenye pampu za vituo vyao waendelee kufanya
hivyo wakati Mamlaka ya Mapato kwa kushirikiana na Wasambazaji na
Uongozi wa TAPSOA wakiendelea kutafuta ufumbuzi wa changamoto
zinazojitokeza za kiufundi na gharama ya Mashine za EFD kwa ajili ya
pampu husika.
(c) Wamiliki/Waendeshaji wote wenye vituo vya
mafuta walio katika kundi la Makampuni ya watu binafsi wanaonunua mafuta
kutoka kwa Makampuni mama na kusambaza/kuuza kwa wateja moja kwa moja
(DODO) ambao hawajafunga Mashine za EFD kwenye pampu waendelee kutumia
Mashine za EFD za kawaida (ETR) wakati changamoto za kiufundi, mtandao
na bei za Mashine za EFD zikishughulikiwa.
Mamlaka ya Mapato kwa
kushirikiana na uongozi wa TAPSOA kwa pamoja tutaendelea kuhimiza
Matumizi ya Mashine za EFD katika vituo vya mafuta vyote Nchini.
Ni vyema kila Mfanyabiashara akatambua wajibu wake na kujenga utamaduni
wa kutekeleza matakwa ya sheria kwa hiari bila kushurutishwa.
0 comments:
Chapisha Maoni