Baraza la Mitihani (NECTA) leo Februari 18, 2016 limetoa Matokeo ya Mtihani wa Kidato cha Nne uliofanyika mwishoni mwa mwaka 2015.
Jumla watahiniwa 272,947 sawa na 67.53% ya watahiniwa waliofanya mtihani wa kidato cha nne 2015 wamefaulu tofauti na mwaka 2014 ambapo ufaulu ulikuwa 68.33%.
Upande wa watahiniwa wa shule, waliofaulu ni 240,996 sawa na asilimia 67.91 ya waliofanya mtihani, wasichana wakiwa 11,125 (64.84) na wavulana wakiwa 124,871 (71.09).
Upande wa watahiniwa wa shule, ufaulu umeshuka kwa asilimia 1.85 ikilinganishwa na mwaka 2014.
Kwa upande wa watahiniwa wa kujitegemea, watahiniwa 31,951 sawa na asilimia 64.80 wamefaulu ikilinganishwa na watahiniwa 29,162 (61.12 waliofaulu mwaka 2014.
Kwa upande wa ubora wa ufaulu kwa kuangalia madaraja waliyopata watahiniwa wa shule, amesema waliopata daraja la Kwanza ni 9,816 sawa na asilimia 2.77, daraja la pili ni 31,986 sawa na asilimia 9.01, daraja la tatu ni 48,127 sawa na asilimia 13.56.
Waliopata daraja la nne ni 240,996 sawa na asilimia 67.91 na waliopata daraja la sifuri (waliofeli) ni 113,489.
Watahiniwa waliopata ufaulu mzuri wa kati ya daraja la kwanza hadi la tatu ni 94,941 sawa na asilimia 24.73 wavulana wakiwa 56,603 sawa na 29.99 na wavulana 38,338 sawa na asilimia 19.63.
Kama bado hujayapata matokeo ya kidato cha nne 2015 bofya >>>HAPA<<<
0 comments:
Chapisha Maoni