Ijumaa, Februari 19, 2016

HADI KUFIKIA MWAKA 2050 NUSU YA WATU WOTE DUNIANI WATAPATA UGONJWA WA MACHO

Kwa mujibu wa tovuti ya habari ya RNS ya Russia, wanasayansi wanakadiri kuwa hadi kufikia mwaka 2050, nusu ya watu wote nduniani watapata mayopia, na mtu mmoja kati ya watano atakabiliwa na hatari ya kupoteza uwezo wa kuona.
Utafiti huo umegundua kuwa, hivi sasa watu bilioni 2 wanasumbuliwa na mayopia, hadi kufikia mwaka 2020 idadi hiyo itaongezeka na kufikia bilioni 2.6, na hadi mwaka 2050 idadi hiyo itakuwa bilioni 5.
Wanasayansi wanasema, mtindo wa maisha na utandawazi wa miji ni chanzo kikuu cha mayopia, na wanashauri kuwa, kutembea kwa muda usiopungua saa mbili nje kila siku kutapunguza hatari ya kupata mayopia.

0 comments:

Chapisha Maoni