Wacha sasa tuangalie suala la ndoa zetu, na aina ya ndoa ambazo zimetuunganisha na tuwapendao. Kila mtu anayo story ya mapenzi ambavyo alishawishika kuwa na huyo ampendaye, na katika hili huwa kila mtu anakosa kujiuliza pengine kwa kutojua nia aina gani ya ndoa anayoitumikia, hizi hapa:
Hapa ni ile true love ambayo wote mnajikuta mmependana na hatimaye kuamua kuwa mke na mme
2.Ndoa za Kulazimisha
Hizi ni zile ndoa binti anaweza kuamua kubeba ujauzito na kutumia kama kigezo cha kuolewa
Na mwanaume anaamua kuoa kwa sababu tu hana namna (Hapa mnaweza kuongeza maana sababu ni nyingi sana.
3.Ndoa za kutamaniana.
Mmeajikuta katika tamaa za kimwili mmeendelea na kutamaniana hatimae inafikia hatua mnawekana ndani..
Matamanio yakiisha kasheshe zinaanza
4. Ndoa za Madawa
(msinipige mawe heheh)Hizi mambo zipo bwana vibinti vya siku hizi vinakamata watu kwa kuwatumia kalumanzira basi dawa zikishindikana kurenew kasheshe zinaanza ndani ya nyumba..mara ooh mara eeh.
5. Ndoa za kuoneana huruma- By PakaJimmy
Unakuta binti anakusimulia maisha aliyopitia...magumu sana, na hakika anatamani asingezaliwa!..
Ukimsikiliza kwa umakini waweza kata shauri kumuoa!
6.Ndoa ya kudimba dimba. By Ashadii
Nje hawa watu ni perfect couple... Ila humo ndani kila mtu na maisha yake; wanakua tu na an understanding, kama mtu anafanya upuuzi iwe mbali na isijulikane na vice versa. Mara nyingi hii inakua as a result ya kuchokana kabisa na kutopendana na wote wakakubali hali halisi. Hivo badala ya kuondoka hapo na kuanza upya wanaona waendelee kushare hasa vile walivochuma pamoja ili mradi nje wasijue hilo.
Umeifahamu ainna ya ndoa unayoitumikia? kama hutojali acha comment yako hapa tujue ni aina gani ya ndoa uliyonayo na chanzo chake
0 comments:
Chapisha Maoni