Southampton wamekataa dau la pauni milioni 8 kutoka Liverpool la kumtaka mshambuliaji Shane Long, 29 (Daily Mirror), beki wa kulia wa Arsenal, Mathieu Debuchy anasema anajuta kuhamia Emirates, na anapanga kuondoka kwenye dirisha hili la usajili (L'Equipe), Debuchy amesema tayari amezungumza na meneja wa Aston Villa, Remy Garde kuhusu uwezekano wa kuhamia Villa Park (Daily Mirror), Arsenal wamempa kazi 'msaka vipaji' wa Leicester aliyesaidia kusajili wachezaji kama Riyad Mahrez na N'Golo Kante (Daily Telegraph), Atletico Madrid wanataka kumrejesha mshambuliaji wao wa zamani anayeichezea Chelsea, Diego Costa. Costa alihamia Stamford Bridge mwaka 2014 kwa pauni milioni 32 (Fichajes), kuumia kwa Costa kwenye ugoko kwenye mchezo dhidi ya Everton siku ya Jumamosi, huenda kukaharakisha usajili wa Alexandre Pato, 26, kutoka Corinthians kwenda Darajani (Daily Telegraph), Newcastle wamepewa nafasi ya kumsajili kiungo wa AC Milan Pato, pamoja na mshambuliaji wa Swansea Bafetimbi Gomis, 30 (Evening Chronicle), hata hivyo Gomis huenda asiuzwe kwenda Newcastle kwa sababu Swansea hawataki kuuza mchezaji kwa timu inayopambana kutoshuka daraja kama wao (South Wales Evening Post), meneja wa Chelsea, Guus Hiddink anasema ingekuwa uamuzi wake, angempa mkataba mpya nahodha John Terry, 35 (Independent), Terry ana uhakika ataongezewa mkataba wa mwaka mmoja baada ya kumalizika kwa msimu huu (Guardian), Tottenham wanapanga kumfuatilia mshambuliaji wa Fulham, Moussa Dembele, 19, lakini meneja wa Fulham Slavisa Jokanovic amesema hataki kumuuza (London Evening Standard), beki wa kushoto wa zamani wa Chelsea na Arsenal, Ashley Cole, 35, amekubali mkataba wa kujiunga na LA Galaxy ya Marekani akitokea Roma (Daily Mail), FC Porto hawana mpango wa kumuuza Yacine Brahimi kwenda Crystal Palace, kufuatia taarifa kuwa mchezaji huyo kutoka Algeria anahamia EPL (A Bola), Leicester City wamesaini mkataba wa pauni milioni 5 na FC Copenhagen kumsajili kiungo mkabaji Daniel Amartey, 21 (Leicester Mercury), beki wa Leeds United Sam Byram, 22, amefanya vipimo vya afya kwenda Everton na atatambulishwa rasmi siku ya Jumatatu (Daily Star), Steven Naismith wa Everton amekubali kujiunga na Norwich kwa mkataba wa pauni milioni 8. Everton sasa wataweza kuziba nafasi yake kwa kumnunua winga kutoka Dynamo Kiev, Andriy Yarmolenko, 26 (Daily Mirror), mshambuliaji wa Southampton Graziano Pelle, 30, anatarajia kuondoka, kufuatia kusajiliwa wa Charlie Austin, 26, kutoka QPR (ESPN), Sunderland bado wapo kwenye mazungumzo ya kumsajili beki wa Lorient, Lamine Kone, 26 (Suderland Echo), mkurugenzi mmoja wa zamani wa michezo wa Barcelona anasema timu hiyo ilitaka kumsajili Sergio Aguero kutoka Manchester City, lakini badala yake wakaamua kumsajili Luis Suarez (Marca), Real Betis wanataka kumchukua meneja wa zamani wa Tottenham na Real Madrid, Juande Ramos, baada ya kufukuzwa kazi kwa Pepe Mel (AS), beki wa kulia wa Manchester City, Pablo Zabaleta, 31, amesema huenda akaondoka mwisho wa msimu na pengine kuelekea Italia (Sun), Manchester City wapo tayari kupanda dau kumsajili kiungo mkabaji wa West Ham, Reece Oxford, 17 (Sun).
Salim Kikeke
0 comments:
Chapisha Maoni