Alhamisi, Januari 07, 2016

SHERIA KUMBANA MUAFRIKA KUSINI ALIYETOA UJUMBE WA KIBAGUZI KATIKA FACEBOOK

Afisa wa serikali ya Afrika Kusini ambaye aliweka ujumbe kwenye mtandao wa Facebook akitoa wito kwa waafrika kuwafanyia wazungu vile Hitler alivyowafanyia wayahudi ataadhibiwa vilivyo.
Hatua za kinidhamu tayari zimechukuliwa dhidi ya afisa huyo ambaye anafanya kazi katika mkoa wa Guateng kwenye idara ya michezo, sanaa, utamaduni na burudani, idara hiyo ilisema.
Mapema hii wiki, afisa huyo kwa jina Velaphi Khumalo aliweka ujumbe kwenye mtandao wa Facebook akisema, "nataka kufukuza wazungu wote humu nchini. Ni lazima tuchukue hatua kama alivyofanya Hitler kwa wayahudi."
Haya yanajiri huku mzozo wa ubaguzi wa rangi ukiwa unaendelea nchini humo baada ya mwanabiashara mzungu Penny Sparrow kuwaita 'tumbili' waafrika waliokuwa wakisherehekea mwaka mpya mjini Durban.

0 comments:

Chapisha Maoni