Waziri wa Elimu wa Uingereza ameunga mkono suala la kupiga marufuku vazi la niqabu na burqa katika shule za nchi hiyo.
Nicky Morgan, Waziri wa Elimu wa Uingereza ameeleza kuwa anaziunga mkono taasisi za elimu ambazo zinataka kupiga marufuku vazi la burqa na niqabu nchini humo. Bi Morgan ameongeza kuwa marufuku hiyo inaweza kutekelezwa kwa wanafunzi na walimu pia. Waziri wa Elimu wa Uingereza ameyasema hayo katika hali ambayo vazi la hijabu ya Kiislamu halijapigwa marufuku katika shule za nchi hiyo .
David Cameroon, Wazirii Mkuu wa Uingereza juzi alikariri kuwa hataki kuwekwa sheria kitaifa kama ilivyo nchini Ufaransa kuhusu vazi la hijabu, hata hivyo akasema anaziunga mkono baadhi ya taasisi au idara za kielimu zilizopiga marufuku burqa na niqabu.
0 comments:
Chapisha Maoni