Jumapili, Januari 17, 2016

NINI UNATAKIWA KUFANYA UKIKUTANA NA AJALI?

Iwapo umehusika kwenye ajali au umesimama kusaidia:
1. Wape tahadhari madereva wa magari mengine kwa kuwasha taa zako za tahadhari ya hatari (indiketa mbili) na, ikibidi, waashirie madereva wengine wapunguze mwendo-dhibiti magari ili kuepuka ajali nyingine – waombe madereva wengine na wanakijiji wakusaidie kufanya hivi
(i)Waombe madereva kuzima injini zao na sigara zozote
(ii)Wasiliana na Polisi mara moja – waeleze eneo hasa la ajali na idadi ya magari na idadi ya watu waliojeruhiwa – waombe watu wengine kufanya hivi ili kuhakikisha kuwa ujumbe umefika.
(iii)Jiandae kutoa huduma ya kwanza – iwapo majeruhi wameumia sana, na kuna matumaini madogo ya kupata msaada haraka, fanya utaratibu wa kuwapeleka majeruhi kwenye hospitali ya karibu
(iv)Wahudumie walioathirika na mali zao – na mshawishi kila mmoja kufanya hivyo.
(v)Usichukue sheria mikononi mwako – usiruhusu watu wampige aliyesababisha ajali.
2. Ukiyaona magari yamesimama mbele, punguza mwendo na uwe tayari kusimama. Iwapo ukiona tayari kuna watu wa kutosha wanaotoa msaada usisimame na kusababisha msongamano. Wakati unapita mahali penye ajali usibabaike – kuwa makini na barabara mbele yako. Fuata amri za maofi sa wa Polisi walio kwenye tukio, na kuwa mvumilivu iwapo kutakuwa na kukaa kwa muda mrefu.
3. Iwapo umehusika kwenye ajali na mtu amejeruhiwa LAZIMA utoe jina na anwani yako (na jina na anwani ya mmiliki wa gari, kama ni tofauti) kwa mtu yeyote aliyehusika na LAZIMA utoe taarifa ya ajali kwenye kituo cha polisi cha karibu au kwa ofi sa wa polisi haraka iwezekanavyo (na kamwe isiwe zaidi ya saa 12 baada ya ajali. Taarifa itawasaidia Polisi, waendesha mashtaka, na Kampuni za Bima kubainisha kilichotokea na iwapo kuna mwenye kosa ambaye anatakiwa kufi dia gharama.
4. LAZIMA usimame na kuwasaidia watu waliojeruhiwa kwenye ajali, isipokuwa kama unahofi a usalama wako. Iwapo umehusika kwenye ajali ya barabarani ambapo hakuna aliyejeruhiwa huhitaji kutoa taarifa Polisi, lakini LAZIMA utoe jina na anwani yako (na jina na anwani ya mmiliki wa gari, kama ni tofauti) na namba ya usajili ya gari lako kwa mtu mwingine yeyote aliyehusika.
Endesha salama, Okoa Maisha

0 comments:

Chapisha Maoni